Maisha
Maisha
ni muda wa kukutana na shida.
Kwa hio, ukipata chakula na soda
Usitafute vitu vingine
Tena kama wewe ni mwembamba, usitake kua mnene.
Lakini tena, usitazame mbele,
Hangalia karibu na we, furahi kwa kitu chochote umesha
pata tena piga vigelegele
Badala ya kufikilia kuhusu maisha ya kesho au kulia na
kupiga kelele.
Usiogopi maisha
Kwa
sababu chini, vitu vyote vitaisha.
Jua
kwamba, ijapokuwa maisha ni magumu
Ukipata
mazuri, hayatapotea kama gurudumu.
Usitafute
kushikana mieleka na maisha
Ili
ubute shida zinazokusumbua kuishiwa au kuisha
Wala
usitumie nguvu zako ili upate uzima
Lakini
ni lazima
Ufanye
kila kitu kwa imani, yaani akili
Tena
kabla ya kuitikia, fikili
Kwa
hio, utapata kitu chochote unachotaka
Kwa
sababu umetumia akili kali kama sungura alikuwa anadanganya paka.
Ndugu
yangu, mimi ni mtungaji wa mashairi
Kukwambia
ukweli sio siri.
Ninataka
nikwambie kwamba maisha ni noma.
Kila
siku kila mutu mzima na kilema
Huamuka
alfajiri
Wakaenda
kupigana na maisha pia wakakutana na shida tofauti
Lakini
wanyama na wadudu hawaatii wasiwasi kukusu maisha, hivyo hivyo inavyofanya miti
Mwenzangu,
jua kwamba maisha ni kama uwanja wa vita
Kila
muda ni kupigana na tabu tofauti na kuendelea kutafuta
Kupata bahati ya kuisha mda mdogo
Na kuondoa kidogo
Shida zinazotuzingatia dimbwi ya maovu
Ili tuwe werevu
Tuonekane kavu.
Maisha si kitu cha kupatwa ovyo au kinyume cha sheria
Maisha ni kitu kinachopangwa na kucheka na kulia
Maisha ni kutembea, kuporomoka, kuanguka na kusimama
Maisha
ni ushujaa wa kutafuta kuwa salama.
_Artist Poet Boshir Melcky
Commentaires
Enregistrer un commentaire